• HABARI MPYA

    Tuesday, June 10, 2014

    MABINGWA WA DUNIA HISPANIA WATUA BRAZIL TAYARI KUTETEA MWALI WAO

    KIUNGO Andres Iniesta na wachezaji wenzake wa Hispania wamewasili Brazil tayari kutetea Kombe la Dunia.
    Iniesta - shujaa wa bao la ushindi katika fainali ya mwaka 2010 alikuwa na wenzake akiwemo Diego Costa a nyota wengine kama Sergio Ramos na Gerard Pique wakati kikosi cha Hispania kinatua Uwanja wa ndege wa Alfonso Pena.
    Baada ya mapokezi mazuri, mabingwa hao wa dunia walipelekwa mjini Curitiba, ambako itakuwa kambi ya Hispania kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Alhamisi. 
    Yuko fiti kweli? Mshambuliaji nyota wa Hispania, Diego Costa (wa tatu mwenye begi) ambaye anahofiwa kuwa bado majeruhi akiteremka kwenye ndege baada ya kutua Brazil
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABINGWA WA DUNIA HISPANIA WATUA BRAZIL TAYARI KUTETEA MWALI WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top