• HABARI MPYA

    Tuesday, June 10, 2014

    KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    MAZISHI ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
    Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.
    Kanali Hassan Mwanakatwe enzi za uhai wake

    TFF imetoa ubani wa sh. 500,000 kwa familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top