MAMBO YALIVYOKUWA SHEREHE ZA TUZO ZA LIGI KUU JANA MASAKI
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba (katikati) akimpongeza mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib (kushoto) kwa kutwaa tuzo ya Bao Bora la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita usiku wa jana ukumbi wa hoteli ya Double Tree By Hilton, Masaki, Dar es Salaam
Mkuu wa Vodacom Kanda Maalum Dar es Salaam, Dominician Mkama (kushoto) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa ubingwa wa Ligi Kuu, Mhasibu wa Yanga, Mike Faidhal (kulia)
Washindi wa tuzo mbalimbali za Ligi Kuu wakiwa na viongozi mbalimbali wa TFF, Waziri Nchemba na Vodacom
Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Ahmed Yahya (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba baada ya timu yake kumaliza nafasi ya pili
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alhaj Muhiddin Ndolanga (kulia) akimkabidhi Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime tuzo ya timu yenye Nidhamu Ligi Kuu
Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko (kulia) akiwa amempakata mwanawe, Shanna Lee pembeni ya mkewe, Bongile Sibanda
Wadau mbalimbali wakifuatilia zoezi hilo jana
Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Ally Suru (kushoto)
Maofisa wa TFF, kutoka kulia Peter Simon, Wilfred Kidau na Pellegrinius Rutayuga
Baadhi wa Waandishi waliohudhuria shughuli hiyo, kutoka kulia Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Mahmoud Zubeiry na Wahariri wa magazeti maarufu ya michezo, Grace Hoka wa gazeti la Bingwa na Willy Moland wa Championi
0 comments:
Post a Comment