SAMATTA ALIVYOPIGA PENALTI YAKE JANA GENK IKISONGA MBELE EUROPA LEAGUE
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ akifunga penalti ya tatu timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji ikishinda kwa penalti 4-2 baada ya sare ya jumla ya 2-2, dhidi ya wenyeji Buducnost jana usiku Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica, Montenegro katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya mchujo wa kufuzu hatua ya makundi ya Europ League.
Samatta akijitayarisha kwenda kupiga penalti yake baada ya mchezo wa jana uliodumu kwa dakika 120 kumalizika kwa wenyeji kushinda 2-0
Kocha wa Genk akiwapa maelekezo wachezaji wake kabla ya zoezi la penalti
Wachezaji wa Genk wakati wa upigwaji wa penalti jana
0 comments:
Post a Comment