YANGA VETERANS WATOA SARE 1-1 NA CHAMAZI KOMBE LA FRESCO
Winga wa Yanga Veterans, Eiphraim makoye akiwatoka mabeki wa Chamazi Veterans katika mchezo wa Kombe la Fresco jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Yanga wakitangulia kwa bao la Aziz Hunter dakika ya 35 kabla ya Chamazi kusawazishia kupitia kwa Anusa Kazembe dakika ya 63
Makoye akipasua katikati ya mabeki wa Chamazi Veterans
Msaliti; Beki wa zamani wa Yanga, Yahya Issa 'Gutta' alichezea Chamazi Veterans jana
Mfungaji wa bao la Yanga jana, Aziz Hunter (katikati) akiwa mawindoni
Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa 'Fusso' (kulia) akimtoka beki wa Chamazi Veterans jana
Benchi la Ufundi la Yanga kutoka kulia Kenneth Mkapa, Omar Kaaya na Abdallah Suleiman Kaaya
Mohammed Hussein 'Mmachinga' (kulia) jana alikosa bao la wazi akiwa amebaki yeye na kipa akaupoeleka mpira jukwaani
Aziz Hunter akiumiliki mpira mbele ya mchezaji mwenzake wa zamani wa Reli ya Morogoro, Yahya Issa
Kiungo wa zamani wa Yanga, Fortunatus Dello Tumba akiwapiga picha wenzake kabla ya mechi
Hiki ndicho kikosi kizima cha Yanga kwa ajili ya mchezo wa jana
0 comments:
Post a Comment