SIMBA SC NA NKANA FC KATIKA PICHA UWANJA WA TAIFA JANA
Kiungo wa Simba SC, Clatous Chama akimuacha chini kiungo wa Nkana FC, Harrison Chisala katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1
Clatous Chama akitoa pasi mbele ya Shadrack Malambo wa Nkana FC. Simba imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza nchini Zambia
Beki Mghana wa Simba, Nicholaus Gyan akipasua katikati ya wachezaji wa Nkana FC
Beki Mkenya wa Nkana FC, Duncan Otieno akiondoka na mpira dhidi ya mshambuliaji Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi
Kocha Mbelgiji wa Simba, Patrick J Aussems akiwa amembeba mchezaji wake Shiza Kichuya
Kocha Patrick Aussems akiwa amekumbatia mfungaji wa bao la tatu, Clatous Chama
Kikosi cha Simba SC kabla ya kuanza kwa mchezo wa jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam
Kikosi cha Nkana FC kabla ya kuanza kwa mchezo wa jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam
Mashabiki wa Simba SC katika mchezo wa jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment