
Mashahidi waliiambia Us Weekly kwamba Brown; “Aliruhusiwa
kuingia ndani, kutoa heshima zake za mwisho na kisha kuondoka. Macho yake
yalikuwa ya njano, akaenda kwenye jeneza kisha na kuondoka. Alikuwa pale kwa dakika
15”.
Kuhusu tetesi kwamba alifukuzwa na uvumi kwamba hakuonekana
kabisa, Brown, ambaye alitarajiwa kutumbuiza kwenye shoo yake moja jana, ametoa
taarifa rasmi akizungumzia sakata zima.
“Mimi na watoto wangu tulikaribishwa kwenye mazishi ya mke
wangu wa zamani Whitney Houston. Tuliketi chini ya ulinzi mkali na baadaye
tukaamriwa kuondoka kwa njia tatu tofauti. Nilishindwa kuelewa kwa nini walinzi
waliifanyia hivi familia yangu na kuendelea kutuuliza, hakuna mwingine pia wa
kuondoka. Walinzi pia walinizuia kwenda kumuona binti yangu Bobbi Kristina (aliyezaa
na Whitney).
Katika mwanga kwenye msiba huo, nikapiga busu jeneza la mke
wangu wa zamani na kuondoka kinyonge. Watoto wangu waliboreka kabisa na tukio hili.
Hii ilikuwa siku ya kumpa heshima Whitney. Nina shaka kama Whitney alitaka haya.
Nitaendelea kumuenzi mke wangu wa zamani katika njia nzuri ninayoijua,” alisema
Bobby.
Mapema wiki hii, chanzo kilisema kwamba hakuna uhusiano mzuri
baina ya ndugu za Houston na Brown, aliyemuoa Houston mwaka 1992, kabla ya
kuachana rasmi mwaka 2007.
“Kuna wana familia wanaofikiri Bobby alimfanya Whitney aingie
kwenye dimbwi la kutumia dawa za kulevya,” chanzo kimoja kilisema. “Lakini sasa
Bobby ni msafi na Whitney kwa bahati mbaya amefariki dunia. Hivyo, kuna chuki,”.
0 comments:
Post a Comment