• HABARI MPYA

    Saturday, February 18, 2012

    CHELSEA MAMBO MAGUMU FA, VILLAS- BOAS ANALO MWAKA HUU

    KLABU ya Chelsea italazimika kucheza tena na Birmingham katika Raundi ya tano ya Kombe la FA, baada ya leo kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, hivyo kuzidi kumuweka katika wakati mgumu kocha Andre Villas-Boas.
    Birmingham ilimpoteza Nahodha wake, Stephen Carr dakika ya 12 aliyeumia, lakini walifanikiwa kupata bao la kuongoza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge dakika nane baadaye kupitia kwa David Murphy.
    Chelsea ilipata penalti dakika ya 22, wakati Wade Elliott alipomchezea rafu Ramires, lakini kipa Colin Doyle aliokoa mkwaju wa Juan Mata.
    Chelsea ililazimika kusubiri hadi dakika ya 62 kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Daniel Sturridge.
    Vyombo vya habari England kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikiripoti kiwamba, kocha Villas-Boas ametofautiana na wachezaji kibao wa timu hiyo wanaopinga mbinu zake za ufundishaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA MAMBO MAGUMU FA, VILLAS- BOAS ANALO MWAKA HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top