• HABARI MPYA

    Saturday, February 18, 2012

    INTER MILAN WAZOMEWA NA MASHABIKI WAO SAN SIRO

    WACHEZAJI wa Inter Milan walijikuta wakizomewa na mashabiki wao wenyewe kwenye Uwanja wa San Siro jana, baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Bologna. Kipigo hiki, ni cha tano katika mechi sita ambazo hawajashinda hata moja na pia ni mechi ya tano wanacheza bila kufunga hata bao moja. Katika mechi hizo sita, Inter imefungwa mabao 15, yenyewe ikifunga manne.
    Hali hii inayohusisha pia kipigo cha mechi ya Kombe la Ligi mbele ya Napoli, inawaweka pabaya katika kuwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, wakishuka hadi nafasi ya sita kwa kuzidiwa pointi sita na Lazio, inayoshika nafasi ya tatu, ambayo iko nyuma kwa mchezo mmoja pia. Mbaya zaidi kwa Napoli, iliifunga 3-0 Fiorentina.
    Mkongwe Marco Di Vaio alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza ndani ya sekunde 60 na Robert Acquafresca akashindilia la mwisho dakika za majeruhi.
    Inter ilipoteza nafasi kibao na kuzidi kumuweka kwenye wakati mgumu, kocha wao Claudio Ranieri.
    Maicon alikosa bao la wazi akiwa yeye na kipa Jean-Francois Gillet na baadaye akapewa pasi na Wesley Sneijder, lakini akapiga juu.
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Diego Forlan, naye alipata nafasi kibao lakini akachemsha.
    Katika mchezo mwingine, Edinson Cavani alikuwa shujaa wa mabao mawili, wakati lingine lilifungwa na Ezequiel Lavezzi, Napoli ikipata jaribio zuri kabla ya kuivaa Chelsea katika Ligi ya Mabingwa keshokutwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: INTER MILAN WAZOMEWA NA MASHABIKI WAO SAN SIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top