• HABARI MPYA

    Saturday, February 18, 2012

    VIGOGO TFF YA CHINA WAPEWA MAISHA MAREFU JELA KWA UFISADI

    MAKAMU wa rais wa zamani wa Chama cha Soka China, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, kwa kukutwa na hatia ya rushwa na upangaji matokeo.
    Taarifa ya Shirika la Habari China, Xinhua, imesema Yang Yimin amekutwa na hatia ya kujipatia hongo ya yuan Milioni 1.25 (sawa na dola za Kimarekani 200,000) na kutupwa jela kuanzia jana hadi miaka kumi na nusu.
    Mwenzake Yang, kutoka Kamati ya Marefa, Zhang Jianqiang, pia alitupwa jela miaka 12 kwa kukutwa na hatia ya kuchukua hongo ya yuan Milioni 2.73 (dola 433,000).
    Refa Lu Jun, aliyechezesha mechi mbili katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 Korea Kusini na Japan, alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na nusu Alhamisi kwa kupokea rushwa ya dola 130,000 kupanga matokeo ya mechi saba za ligi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIGOGO TFF YA CHINA WAPEWA MAISHA MAREFU JELA KWA UFISADI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top