IMEWEKWA SEPTEMBA 2, 2013 SAA 2:21 ASUBUHI
HATIMAYE uhamisho wa Gareth Bale ulikamilika jana usiku alipotua Real Madrid kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 86.
Baada ya majadiliano marefu yaliyoteka hisia za wengi majira haya ya joto, nyota huyo wa Wales amekubali mshahara wa Pauni 256,000 kwa wiki katika Mkataba wa Miaka sita na leo atafanyiwa vipimo afya kabla ya kutambulishwa mbele ya vyombo vya habari.
Uhamisho wake unapiga bao usajili wa bei mbaya zaidi uliokuwa unashika rekodi kabla yake, wa Cristiano Ronaldo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 80 mwaka 2009 kutoka Manchester United.
Huyu hapa: Mchezaji mpya wa Real Madrid, Gareth Bale akiwa na mashabiki wa timu yake mpya baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Barajas
Safarini: Gareth Bale, aliondoka London Jumamosi na amekamilisha uhamisho wake kutua Real Madrid
Hatimaye kimeeleweka: Bale ameondoka Tottenham baada ya kuichezea katika mechi moja tu ya kujiandaa na msimu