• HABARI MPYA

    Thursday, June 19, 2014

    SUAREZ AIANGAMIZA ENGLAND KOMBE LA DUNIA

    ENGLAND imepoteza mechi ya pili mfululizo ya Kundi D Kombe la Dunia, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Uruguay mjini Sao Paulo, Brazil usiku huu.
    Mbaya wa England usiku huu alikuwa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez aliyefunga mabao yote mawili, moja kila kipindi wakati bao pekee la Three Lions lilifungwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.

    Suarez akishangilia baada ya kuifungia Uruguay bao la pili, huku kipa Joe Hart akisikitika

    Uruguay walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 39, baada ya Luis Suarez kumalizia kazi nzuri ya Cavani.
    England walisawazisha dakika ya 75, Wayne Rooney akimalizia vizuri krosi ya Glen Johnsont. Bao hilo liliwapa tamaa ya mabao zaidi England, na kujikuta wanamsahau kidogo Suarez, ambaye alitumia mwanya huo kuwafunga bao la pili dakika ya 85.
    Suarez alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira mrefu wa juu uliomshinda Nahodha wa England, Steven Gerrard na kumtungua Joe Hart.
    Finally: Rooney runs off after scoring his first World Cup goal and England's equaliser
    Rooney akishangilia baada ya kuifungia bao lililokuwa la kusawazisha England


    Stopped illegally: Sturridge pokes the ball through and Diego Godin (left) handballs it
    Sturridge akihangaika katikati ya mabeki wa Urugu

    Matokeo hayo,  yanaifanya Uruguay ifufue matumaini ya kutinga 16 Bora baada ya kuvuna pointi tatu za kwanza, wakati England sasa inasubiri miujiza tu ili kuweza kuingia hatua ya pili ya michuano hiyo.
    Costa Rica ina pointi tatu sawa na Uruguay wakati England haina pointi sawa na Honduras.
    Kikosi cha Uruguay kilikuwa: Muslera, Gimenez, Godin, Caceres, Pereira/Fucile dk79, Lodeiro/Stuani dk67, Gonzalez, Arevalo Rios, Rodriguez, Cavani na Suarez/Coates dk89.
    England: Hart, Baines, Cahill, Jagielka, Johnson, Gerrard, Henderson, Sterling/Barkley dk64, Rooney, Welbeck/Lallana dk71 na Sturridge.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AIANGAMIZA ENGLAND KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top