MWANASOKA wa kimataifa wa Ivory Coast, Serey Die leo ameonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake baada ya kuichezea dhidi ya Colombia licha ya taarifa za msiba wa baba yake mzazi saa mbili kabla ya mechi.
Kiungo huyo mwenye kipaji alianza kulia wakati wimbo wa taifa wa Ivory Coast unachezwa kabla ya mchezo huo wa Kundi C game, ambao timu yake ililala 2-1.
Wengi walidhani Die alimwaga machozi kwa sababu ya kufikiria ugumu atakaokabiliana nao uwanjani, pamoja na hayo ikabainika kwamba baba wa mchezaji huyo mwenye umri 29 amefariki dunia muda mfupi kabla ya mchezo huo uliofanyika Brasilia.
Huzuni: Kiungo wa Ivory Coast, Serey Die akimwaga machozi wakati wimbo wa taifa wa nchi yake unachezwa
Die alijitahidi kujisahaulisha hali hiyo na kuimba mane no ya wimbo wa taifa lake, lakini akashindwa kuzuia machozi yake.
Beki Serge Aurier na mchezaji wa zamani wa Tottenham, Didier Zokora haraka sana walimzingira Die kumfariji kabla ya mchezo kuanza.
Bahati mbaya zaidi matokeo ya mchezo huo hayakuwa mazuri kwa Ivory Coast timu hiyo ya Didier Drogba ikifungwa 2-1 mabao ya James Rodriguez na Juan Fernando Quintero, huku mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho akiifungia timu hiyo ya Afrika Magharibi bao la kufutia machozi.
Die aliendelea kuwa mwenye huzini hadi wakati wa mchezo
0 comments:
Post a Comment