• HABARI MPYA

    Tuesday, June 10, 2014

    SUAREZ NA URUGUAY AWASILI BRAZIL AKIONEKANA FITI KABISA KAMA CAVANI

    KIKOSI cha Uruguay kimetua Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia na mshambuliaji Luis Suarez amewasili nao akionekana kuwa fiti na tayari kuwasha moto.
    Timu hiyo ya Amerika Kusini imetua mjini Belo Horizonte jana, kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kuwania Kombe la michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.
    Uruguay inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo Jumamosi dhidi ya Costa Rica, kabla ya kumenyana na England na Italia katika mechi nyingine za Kundi D.
    Wamewasili: Luis Suarez akiwasili Brazil na kikosi cha Uruguay na juu yake ni mshambuliaji pacha wake, Edinson Cavani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ NA URUGUAY AWASILI BRAZIL AKIONEKANA FITI KABISA KAMA CAVANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top