• HABARI MPYA

    Friday, March 20, 2015

    AZAM TV WAPENYEZA KENYA KWA FUJO; NI MIKWANJA TU

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    AZAM TV wamepenyeza Kenya na kutia mkataba wa miaka mitatu wa kima cha milioni 2.25 dola za Marekani kupeperusha mechi za ligi kuu ya Shirikisho la Soka Kenya, FKF PL.
    Wakizindua ufadhili huo katika hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi mchana wa leo – Ijumaa Machi 20, Azam kupitia kwa katibu mkuu mtendaji Rhys Torrington, jumla ya elfu 750 000 dola za Marekani zitatolewa kwa msimu huku vilabu vinyavyoshiriki ligi hiyo vikitia kibindoni kitita cha shilingi milioni moja pesa za Kenya kila mwezi.
    Kwa mujibu wa mkataba huo, mechi mbili zitapeperushwa kwa juma kwanzia wiki ijayo kupitia ving’amuzi hivyo huku runinga moja ya nchini Kenya pia ikiruhusiwa kuonyesha mechi hizo pindi tu watakapoafikiana na FKF.
    FKF ilianzisha ligi yake kuu yenye timu 18 baada ya kuvunja ndoa yao na kampuni inayosimamia ligi kuu, KPL, kuhusu idadi ya timu msimu huu. KPL, walizitaka 16 huku FKF kupitia rais Sam Nyamweya wakipiga kampeni ya timu 18, jambo ambalo limetimizwa.
    Hata hivyo, ligi kuu ya KPL inaendelea timu 16 zikishiriki, wote wakiwa na ufadhili vile vile.
    Shabana FC, Kakamega Homeboyz, Zoo Kericho, Ligi Ndogo SC, West Kenya Sugar, Agrochemicals, Oserian FC, Finlays Horticulture, FC Talanta, Bidco United, Nairobi Stima, Modern Coast Rangers FC, Posta Rangers FC, Nakumatt FC, MOYAS FC, Kariobangi Sharks, St. Joseph FC na AFC Leopards vinacheza ligi hiyo japo Leopards hawajashiriki mechi yoyote na huenda nafasi yao ikachukuliwa na Nzoia United.

    Rais wa FKF Sam Nyamweya akiwa na Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington katika uzinduzi wa ufadhili wa FKF PL

    Orodha ya mechi za wikiendi kwenye FKF PL
    Jumamosi
    Oserian FC Vs Nakumatt – Oserian
    Agrochemical Vs Zoo Kericho – Kisumu
    Kakamega Homeboyz Vs St. Joseph – Bukhungu, Kakamega
    FC Talanta Vs Modern Coast – Kasarani
    Jumapili
    Posta Rangers Vs Finlays Horticulture – Thika
    West Kenya Vs Nairobi Stima – Bukhungu, Kakamega
    Kariobangi Sharks Vs Ligi Ndogo – City Stadium
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM TV WAPENYEZA KENYA KWA FUJO; NI MIKWANJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top