UGANDA YATANGULIZA MGUU MMOJA CHAN YA RWANDA, YAICHAPA SUDAN 2-0
Uganda imeanza vizuri hatua ya mwisho ya mchujo wa kufuzu Michano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuifunga mabap 2-0 Sudan jana Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala.
Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Frank Kalanda na Nahodha Farouk Miya na sasa The Cranes itahitaji sare au kufungwa si zaisi ya 1-0 katika mchezo wa marudiano ili kufuzu CHAN ya 2016 nchini Rwanda.
0 comments:
Post a Comment