• HABARI MPYA

    Wednesday, November 04, 2015

    MECHI YA SIMBA NA YANGA NANI MTANI JEMBE YAFUTWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHEZO maarufu wa kila mwaka baina ya watani jadi, Simba SC na Yanga SC hautakuwapo mwaka huu, imefahamika.
    Habari za kiuchunguzi ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imezipata kutoka kwa waandaaji wa mchezo huo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mchezo huo mwaka huu hautakuwapo.
    Hata hivyo, sababu haswa za kufutwa kwa mchezo huo mwaka huu hazijulikani, ingawa vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa Taifa uliofanyika mwezi uliopita limehusishwa.
    Viungo wa zamani wa Simba, Amri Kiemba (kulia) na Athumani Iddi 'Chuji' (kushoto) wakichuana katika Nani Mtani Jembe ya kwanza mwaka juzi

    “Mchakato wa uchaguzi ulisababisha mambo yote yasimame na hadi sasa naweza kukuthibitishia, mechi ya Nani Mtani Jembe mwaka huu haipo,”kimesema chanzo kutoka TBL.
    Bado haijulikani mustakabali wa mchezo huo kwa mwakani na TBL ambao ni wadhamini wa Simba SC na Yanga SC kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kulitolea ufafanuzi hilo.
    Mchezo wa Nani Mtani Jembe ambao mwaka huu ulitarajiwa kuingia katika msimu wake wa tatu, tayari umejiziloea umaarufu baada ya miaka miwili ya kufanyika kwake awali.
    Na Simba SC imekuwa na bahati na mechi hiyo baada ya kushinda mara zote mbili, Desemba 23 mwaka juzi 3-1 mabao yao yakifungwa na Amisi Tambwe mawili moja kwa penalti na Awadh Juma, la Yanga SC likifungwa na Emmanuel Okwi- na Desemba 13 mwaka jana walishinda 2-0 mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA SIMBA NA YANGA NANI MTANI JEMBE YAFUTWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top