TIMU ya Mbeya City ya Mbeya inataka kusajili wachezaji watano katika kipindi cha dirisha dogo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kinachoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara imeelezwa.
Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdul Mingange, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba hayo ndiyo mapendekezo aliyowasilisha na anaamini akipata wachezaji hao, timu yao itarejesha makali yake.
Mingange alisema kwamba katika usajili huo mpya anahitaji kuongeza washambuliaji watatu na mabeki wawili.
"Nimeandika katika ripoti yangu kuwa, nahitaji wachezaji watano wapya ambao tukiwaongeza, mambo yatakuwa mazuri na Mbeya City itarejesha makali yake waliyoanza nayo kwenye ligi kuu," alisema Mingange.
Aliongeza kuwa katika mechi walizocheza, kikosi chao kilionekana wazi safu yake ya ushambuliaji na ulinzi haikuwa imara.
Alisema kwamba baada ya mapumziko ya wiki mbili, wachezaji wake watarejea mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuendelea na mazoezi na wanaamini watakuwa na nguvu mpya.
"Tunahitaji kucheza kwa bidii ili kujikwamua, nafasi tuliyoko katika msimamo wa ligi si nzuri," Mingange alisema.
Mbeya City yenye pointi tisa na iko katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi imecheza mechi 10 na kushinda mbili na kutoka sare mara tatu huku ikipoteza michezo mitano.

![]() |
Basi la Mbeya City linahitaji abiria watano wapya kwa mujibu wa kocha Mingange |
"Nimeandika katika ripoti yangu kuwa, nahitaji wachezaji watano wapya ambao tukiwaongeza, mambo yatakuwa mazuri na Mbeya City itarejesha makali yake waliyoanza nayo kwenye ligi kuu," alisema Mingange.
Aliongeza kuwa katika mechi walizocheza, kikosi chao kilionekana wazi safu yake ya ushambuliaji na ulinzi haikuwa imara.
Alisema kwamba baada ya mapumziko ya wiki mbili, wachezaji wake watarejea mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuendelea na mazoezi na wanaamini watakuwa na nguvu mpya.
"Tunahitaji kucheza kwa bidii ili kujikwamua, nafasi tuliyoko katika msimamo wa ligi si nzuri," Mingange alisema.
Mbeya City yenye pointi tisa na iko katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi imecheza mechi 10 na kushinda mbili na kutoka sare mara tatu huku ikipoteza michezo mitano.
0 comments:
Post a Comment