KIUNGO wa Italia, Riccardo Montolivo yuko hatarini kukosa Kombe la Dunia baada ya kuvunjika mguu jana Uwanja wa Craven Cottage timu yake ikitoka safe ya bila kufungana na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kirafiki.
Montolivo alikuwa Nahodha wa kikosi cha kocha Cesare Prandelli aliyewapumzisha nyota wake kibao wenye majina makubwa akiwemo Mario Balotelli kabla ya mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia dhidi ya England nchini Brazil Juni 14.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alicheza kwa dakika 13 tu kabla ya kugongwa na Alex Pearce mbele ya macho ya kocha wa England, Roy Hodgson na Gary Neville, waliokuwa wakishuhudia mchezo huo katika boksi la Wakurugenzi wa Fulham.
Pole kiongozi: Nahodha wa Italia jana, Riccardo Montolivo aliumia katika mchezo wa kirafiki na Jamhuri ya Ireland
Nyota benchi: Mario Balotelli alikuwa benchi jana
0 comments:
Post a Comment