SIMBA NA YANGA B ZATUA MBEYA KUSHIRIKI MASHINDANO MAALUM
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (katikati) akimkabidhi Jezi Meneja wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, Mohamed Mposo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI. Makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi ndani ya Ofisi za Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Yanga itaanza na Mbeya City leo jioni, kabla ya Simba kumenyana na Tanzania Prisons kesho na fainali itachezwa Jumamosi kwa kuwakutanisha washindi wa mechi za leo na kesho. Kushoto ni Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.
Meneja wa timu ya Mbeya City, Geofrey Katepa akipokea vifaa
Meneja timu ya Simba B, Nico Nyagawa (wa pili kulia) akipokea vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.
Meneja timu ya Tanzania Prisons, Havinitishi Abdallah akipokea vifaa vya michezo
0 comments:
Post a Comment