• HABARI MPYA

    Tuesday, November 03, 2015

    SIMBA SC WAPEWA SIKU 17 ZA MAPUMZIKO, WAKIRUDI WANA AZAM

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Simba SC iimewapa mapumziko mafupi ya siku 17 wachezaji wake wakati huu ambao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imesimama kwa muda.
    Taarifa ya Simba SC imesema kwamba wachezaji wote wameshauriwa kuendelea kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuiweka miili katika utayari wa kimchezo wakati wote.
    Aidha, taarifa imesema kwamba kocha Muingereza wa timu hiyo, Dylan Kerr amewapa mwongozo wachezaji wa timu hiyo juu ya namna ya kujitunza katika kipindi hiki.
    “Tumewapa likizo fupi wachezaji, ingawa hawaendi kupumzika kabisa, kwani kila mmoja amepewa karatasi inayomuelekeza nini cha kufanya kila siku, na watakaporudi kila mmoja atafanya jaribio kulingana na maelezo yaliyopo kwenye karatasi,”imemnukuu kocha Kerr taarifa hiyo.
    Kocha wa Simba SC, Dylann Kerr (kushoto) na wasaidizi wake
     

    Kerr amesema mazoezi ambayo wanakwenda kuyafanya wakiwa katika kipindi hichi cha mapumziko ni mazoezi ya viungo zaidi. Kwa upande wake, Nahodha Mussa Hassan Mgosi amewataka wachezaji wenzake kuzingatia mazoezi hayo, kwani ndiyo mtaji wa ushindi.
    “Napenda kuwasisitiza wachezaji wenzangu, kufuatatilia na kuzingatia ratiba ya mazoezi ambayo tumepewa na kocha Kerr, lazima kila mtu akirudi awe fiti kuliko alivyo sasa,”amesema Mgosi.
    Ligi Kuu imesimama kupinda maandalizi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo katikati ya mwezi huu itakuwa na mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria na itakaporejea mchezo wa kwanza wa Simba SC dhidi ya utakuwa dhidi ya vinara, Azam FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAPEWA SIKU 17 ZA MAPUMZIKO, WAKIRUDI WANA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top