• HABARI MPYA

    Tuesday, November 03, 2015

    YANGA SC WAPEWA MAPUMZIKO MAFUPI, KUINGIA KAMBINI NOVEMBA 12

    MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Desemba 12, 2015
    Kagera Sugar Vs Ndanda FC
    Stand United Vs Mwadui FC
    Mbeya City Vs Mtibwa Sugar
    Azam FC Vs Simba SC
    Majimaji FC Vs Toto Africans
    Mgambo JKT Vs Yanga SC
    Desemba 13, 2015
    JKT Ruvu Vs Prisons
    Coastal Union Vs African Sports
    Yanga SC wamepewa mapumziko hadi Novemba 12, mwaka huu

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    UONGOZI wa Yanga SC umetoa mapumziko ya wiki moja na ushei kwa wachezaji wake hadi Novemba 12, mwaka huu baada ya kusimama kwa muda kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba baada ya mapumziko hayo wachezaji watakutana na moja kwa moja kuingia kambini kwa ajili ya michezo ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
    “Tumetoa mapumziko hadi tarehe 12, wachezaji ambao hawapo timu ya taifa watarudi siku hiyo na moja kwa moja timu itaingia kambini, kwa wale ambao wapo timu ya taifa wataripoti baada ya tarehe 17,”amesema Muro.
    Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria.
    Taifa Stars ambayo imeweka kambi Afrika Kusini tangu jana, Novemba 14 itaikaribisha Algeria mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana mjini Algiers Novemba 17 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
    Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea Desemba 12, mwaka huu, Kagera Sugar wakiikaribisha Ndanda FC, Stand United na Mwadui, Mbeya City na Mtibwa Sugar, Azam FC na Simba SC na Majimaji na Toto Africans, wakati Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Yanga SC na Desemba 13, JKT Ruvu wataikaribisha Prisons na Coastal Union watamenyana na African Sports.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAPEWA MAPUMZIKO MAFUPI, KUINGIA KAMBINI NOVEMBA 12 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top