CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimeagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura kujadili mwenendo wa Kamati ya Utendaji na mambo mengine kadhaa.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa ZFA kilichofanyika leo katika Hoteli ya Courtyard mjii Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Kikao kimefuatia tishio la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuifungia Zanzibar kwenye soka ya kimataifa baada ya kufikishana Mahakamani, jambo ambalo ni kinyume na sheria za FIFA.
Kikao hicho cha usuluhishi kilichohusisha pande zote zinazovurugana, kimeagiza pia Mkutano wa dharula upokee taarifa ya Mapato na matumizi ya ZFA, kuteua kamati ndogo ya kuandika upya Katiba ya ZFA na Kamati ya sasa inayoendesha ligi Zanzibar iongezewa wajumbe watatu watakoteuliwa na Rais wa ZFA.
Kikao kimeagiza Rais wa ZFA, Ravia Idarus, kwa mujibu wa Katiba ya ZFA, ndiye aitishe Mkutano huo.
"Ili maamuzi haya yaweze kuwa na nguvu za kisheria na kikatiba, kikao kimeazimia kuwa mashauri yote yaondolewe Mahakamani sasa na waliohusika kufungua mashtaka hayo wamekubali kuyaondoa mara moja,"imesema taarifa ya TFF.

![]() |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi kulia amesuluhisha mgogoro wa ZFA |
Kikao hicho cha usuluhishi kilichohusisha pande zote zinazovurugana, kimeagiza pia Mkutano wa dharula upokee taarifa ya Mapato na matumizi ya ZFA, kuteua kamati ndogo ya kuandika upya Katiba ya ZFA na Kamati ya sasa inayoendesha ligi Zanzibar iongezewa wajumbe watatu watakoteuliwa na Rais wa ZFA.
Kikao kimeagiza Rais wa ZFA, Ravia Idarus, kwa mujibu wa Katiba ya ZFA, ndiye aitishe Mkutano huo.
"Ili maamuzi haya yaweze kuwa na nguvu za kisheria na kikatiba, kikao kimeazimia kuwa mashauri yote yaondolewe Mahakamani sasa na waliohusika kufungua mashtaka hayo wamekubali kuyaondoa mara moja,"imesema taarifa ya TFF.
0 comments:
Post a Comment