• HABARI MPYA

    Tuesday, November 03, 2015

    ESTHER 'LUNYAMILA' ATUNGIKA DALUGA, KUAGWA RASMI JUMAMOSI CHAMAZI

    Esther Chaburuma 'Lunyamila' enzi zake alikuwa moto wa kuotea mbali
    MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ Esther Chaburuma ‘Lunyamila’ ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Malawi utakaochezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
    Chaburuma amekua ni miongoni mwa wachezaji waasisii wa Twiga Stars ambapo amekua akiitumikia timu hiyo tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa timu inapojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma amesema wameamua kutumia mchezo huo wa kirafiki kwa ajili ya kumuaga Chabruma ambaye amekua ni chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake, kutokana na kuwafanya wanawake wengi kujitokeza kucheza mchezo huo.
    Naye kocha wa timu hiyo, Rogasian Kaijage amesema vijana wake wapo katika hali nzuri, wananadelea na maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi, ambapo anaimani watautumia vizuri katika kumuaga mchezaji mwenzao wa siku nyingi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ESTHER 'LUNYAMILA' ATUNGIKA DALUGA, KUAGWA RASMI JUMAMOSI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top