Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
AZAM FC imewapa mapumziko wachezaji wake hadi Novemba 25, kufuatia kusimama kwa muda kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba wachezaji wote wanatakiwa kuripoti Novemba 25 kwa ajili ya maandalizi ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
Taifa Stars ambayo imeweka kambi Afrika Kusini tangu jana, Novemba 14 itaikaribisha Algeria mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana mjini Algiers Novemba 17 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Na Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea Desemba 12, mwaka huu, Azam FC wakimenyana na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar wakiikaribisha Ndanda FC, Stand United na Mwadui, Mbeya City na Mtibwa Sugar na Majimaji na Toto Africans, wakati Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Yanga SC na Desemba 13, JKT Ruvu wataikaribisha Prisons na Coastal Union watamenyana na African Sports.
Azam FC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa sasa baada ya kujikusanyia pointi 25 katika mechi tisa, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 23, wakati Mtibwa Sugar yenye pointi 22 ni ya tatu na Simba SC yenye pointi 21 ni ya nne, huku Stand United ikishika nafasi ya tano kwa pointi zake 19.

0 comments:
Post a Comment