![]() |
Festus Mbewe ni tegemeo la Zambia |
Zambia imealikwa kucheza michuano ya mataifa manne itakayofanyika Novemba 6 na 7 mjini Luanda ambako watamenyana na Namibia, DRC na wenyeji Angola.
Michuano hiyo inakuja wiki moja kabla ya Zambia kucheza na Sudan katika mbio za Urusi 2018. "Itakuwa sehemu ya mazoezi yetu na kitu muhimu ni kuwajenga wachezaji wetu kabla hatujacheza na Sudan,"amesema Lwandamina. "Hatuhitaji mechi nyingi kipindi hiki ndiyo maana michuano hii muhimu kwetu," ameongeza.
"Muhimu ni kwamba tutapata mechi fulani za mazoezi na tutawatumia wachezaji wengi kadiri tutakavyoweza, hivyo tutakuwa na fursa nzri ya kuona wa kuchukua,"amesema.
Lwandamina amechukua wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani pekee kwa ajili ya michuano hiuyo na anatarajiwa kupunguza kikosi chake na kubaki na wachezaji 24 kabla ya safari ya Novemba 4.
Wachezaji hao wa nyumbani wameweka kambi Lusaka tangu jana kujiandaa na mechi mbili dhidi ya Sudan wiki ijayo.
Zambia itakuwa mwenyeji wa Sudan katika mchezo wa kwanza Novemba 15 mjini Ndola kabla ya kurudiana siku tatu baadaye na mshindi wa jumla ataingia haua ya makundi kuwania tiketi ya Urusi 2018.
0 comments:
Post a Comment