SERENGETI BOYS NA AMAJIMBOS KATIKA PICHA JANA CHAMAZI
Beki wa Afrika Kusini, Kwenzokuhle Shinga (kulia) akimchezea rafu mshambuliaji wa Tanzania, Mohamed Rashid Abdallah katika mchezo wa marudiano Raundi ya pili kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 17 mwakani nchini Madagascar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Serengeti ilishinda 2-0 na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya wiki iliyopita kutoa sare ya 1-1
Mohamed Rashid Abdallah wa Serengeti Boys akiambaa na mpira pembeni ya beki wa Amajimbos
Shaaban Zubeiry wa Serengeti Boys (kushoto) akimtoka beki wa Amajimbos
Yohanna Nkomola wa Serengeti Boys (kulia) akiwatoka mabeki wa Amajimbos
Israel Patrick Mwenda wa Serengeti Boys akimtoka beki wa Amajimbos
Beki wa Amajimbos akiinua mguu kuondosha mpira kwenye himaya ya Israel Mwenda
Kipa wa Amajimbos,Glen Tumelo Baadjes akiruka kuookoa npira dhidi ya mshmbauliaji wa Serengeti Boys, Shaaban Zubeiry
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na MIchezo, Nape Nnauye (kulia) akifurahia na Rais wa TFF, Jamal Malinzi baada ya bao la pili
0 comments:
Post a Comment