Kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto akituliza mpira kifuani mbele ya kiungo wa JKT Ruvu, Hassan Dilunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo (kulia) akikimbilia mpira dhidi ya beki wa JKT Ruvu, Pera Mavuo
Kipa wa JKT Ruvu, Said Kipao akiwa ameruka juu kudaka mpira mrefu uliotokea pembeni
Beki wa JKT Ruvu, Rahim Juma akimuacha chini mshambuliaji wa Simba SC, Frederic Blagnon
Kiungo wa Simba SC akipasua kwenye msitu wa mabeki wa JKT Ruvu
Salim Aziz Gilla wa JKT Ruvu (kulia) akiuzuia mpira dhidi ya kiungo wa Simba SC, Jamal Mnyate
Beki wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala' akimtoka kiungo wa JKT, Ismail Amour
Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib (kulia) akimtoka beki wa JKT Ruvu, Rahim Juma
0 comments:
Post a Comment