SIMBA SC NA TP MAZEMBE KATIKA PICHA UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI
Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco 'Adebayor' (kulia) akitafuta maarifa ya kumpokonya mpira mchezaji wa TP Mazembe katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam timu hizo zikitoka sare ya 0-0.
Kiungo Mzambia wa Simba, Clatous Chama akipiga krosi pembeni ya beki wa TP Mazembe, Mganda Joseph Ochaya
Beki Mburkinabe wa Simba SC, Zana Coulibaly (kushoto) akimlamba chenga beki wa TP Mazembe, Kevin Mondeko Zatu
Kiungo Mnyarwanda wa Simba, Haruna Niyonzima akimiliki mpira katikati ya Uwanja pembeni ya beki wa TP Mazembe, Godet Masengo
Beki wa Simba, Serge Wawa Pascal (katikati) akimsabahi kipa wa TP Mazembe, Muivory Coast mwenzake, Sylvain Gbohouo
Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed 'Mo' Dewji akizungumza na Rais wa klabu, Swedi Nkwabi
Mashabiki wa Simba SC katika mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumamosi Uwanja wa Taifa
Mashabiki wa Simba SC katika mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumamosi Uwanja wa Taifa
Kikosi cha Simba SC kabla ya mchezo dhidi ya TP Mazembe Jumamosi Uwanja wa Taifa
Kikosi cha TP Mazembe kabla ya mchezo dhidi ya Simba Jumamosi Uwanja wa Taifa
0 comments:
Post a Comment