| Mkurugenzi wa maduka maarufu ya nguo za kijanja ya Zizzou Fashions, Athumani Tippo (mwenye kofia kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo, Nahodha wa Mwanza All Stars, Juma Amir Maftah 'Pele wa Mwanza' juzi Ilemela mjini Mwanza. Wachezaji waliong'ara na timu mbalimbali Mwanza wameungana kuanzisha timu yao, iitwayo Mwanza All Stars na Tippo, mchezaji wa zamani mkoani humo, alirejea nyumbani kutoka Dar es Salaam kwenda kuisaidia vifaa vya mazoezi timu hiyo, ikiwemo seti ya jezi na mipira mitano. |
0 comments:
Post a Comment