Refa Deniz Aytekin akimtoa nje kwa kadi nyekundu, mshambuliaji wa Borussia-Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 72 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu Amine Harit wa Schalke katika sare ya 4-4 kwenye mchezo wa Bundesliga usiku wa Jumamosi Uwanja wa Signal-Iduna-Park mjini Dortmund. Aubameyang alifunga bao la kwanza la Dortmund dakika ya 12 na akaseti la tatu lililofungwa na Mario Gotze dakika ya 20, wakati mabao mengine ya Dortmund yalifungwa na Benjamin Stambouli aliyejifunga dakika ya 18 na Raphael Guerreiro dakika ya 25. Mabao ya Schalke yalifungwa na G. Burgstaller dakika ya 61, A. Harit dakika ya 65, D. Caligiuri dakika ya 86 na Naldo dakika ya 90 na ushei PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Bruno Fernandes and Iliman Ndiaye come to blows in fiery clash as Everton
hold Man United to 2-2 draw in Atlanta
-
The flashpoint occurred just before Everton's second equaliser. Fernandes
slid in from behind on Ndiaye near the halfway line, prompting an angry
reaction ...
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment