YANGA NA TANZANIA PRISONS KATIKA PICHA JANA CHAMAZI
Kiungo wa ulinzi wa Tanzania Prisons, Jumanne Elfadhili (kulia) akinyoosha mguu juu kuokoa dhidi ya kiungo wa Yanga, Emmanuel Martin (katikati) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona
Beki wa Yanga, Gardiel Michael akimuacha chini mchezaji wa Prisons, Salum Kimenya
Mshambuliaji wa Prisons, Eliuter Mpepo akimtoka beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante'
Beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail akimiliki mpira pembeni ya Gardiel Michael wa Yanga
Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib akiondoka na mpira dhidi ya Eliuter Mpepo wa Prisons
Michael Ismail wa Tanzania Prisons akimdhibiti winga wa Yanga, Emmanuel Martin
Ibrahim Ajib wa Yanga (kulia) na Salum Kimenya wa Prisons wakinyoosha mikono juu kumuuliza refa nani katoa nje mpira
Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina akiwapa maelekezo wachezaji wake jana
Wachezaji wa Tanzania Prisons wakifanya maombi katika lango lao kabla ya mchezo kuanza jana
0 comments:
Post a Comment