Wachezaji wa Manchester United wakirejea katikati kinyonge baada ya Wolves kusawazisha bao katika sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford leo. United walitangulia kwa bao la mchezaji wake mpya, kiungo Frederico Rodrigues Santos 'Fred' dakika ya 18 akimalizia pasi ya Mfaransa Paul Pogba, kabla ya Joao Moutinho kuisawazishia Wolverhampton dakika ya 53 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mmexico, Raul Jimenez. Mchezo huo ulihudhuriwa na kocha wa zamani wa Mashetani Wekundu, Sir Alex Ferguson kwa mara ya kwanza tangu aripotiwe kuugua Mei mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Miyu Yamashita holds off Charley Hull to win first major at Women's Open
-
Home favourite came agonisingly close
31 minutes ago
0 comments:
Post a Comment