Kipa wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris akiokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya mwisho kuinusuru Spurs kuchapwa baada ya kutoa sare ya 1-1 Uwanja wa Wembley leo. Aaron Ramsey alitangulia kuifungia Arsenal dakika ya 16 akimalizia pasi ya Alexandre Lacazette kabla ya Harry Kane kuisawazishia Spurs kwa penalti dakika ya 74 baada ya kuchezewa na rafu na Shkodran Mustafi. Arsenal ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Lucas Torreira aliyetokea benchi kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu Danny Rose. Kwa sare hiyo, Arsenal inafikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 29 ikiangukia nafasi ya tano, wakati Tottenham inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 61 za mechi 29 pia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
FIFA hit by 'major class-action lawsuit' by players' group who are seeking
BILLIONS in compensation over transfer rules after EU law breach last year
-
A group of current and former footballers are reportedly set to take legal
action against FIFA over the world football governing body's current
transfer ru...
12 minutes ago
0 comments:
Post a Comment