Beki Marcos Rojo akikimbia kushangilia kishujaa huku amedandiwa mgongoni na Nahodha wake, Lionel Messi baada ya kuifungia Argentina bao la ushindi dakika ya 86 ikiilaza Nigeria 2-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Dunia leo Uwanja wa Saint-Petersburg nchini Urusi. Argentina ilitangulia kwa bao la Messi dakika ya 14, kabla ya Victor Moses kuisawazishia Super Eagles kwa penalti dakika ya 51, kufuatia Javier Mascherano kumshika hadi kumungusha Leon Balogun kwenye boksi wakati wa kona. Lakini refa Cuneyt Cakir aliingia lawamani kwa kuwanyima penalti ya pili Nigeria, huku Argentina ikienda hatua ya 16 Bora kama mshindi wa pili wa kundi kwa pinti zake nne nyuma ya Croatia, iliyomaliza na pointi tisa. Argentina itamenyana na Ufaransa Juni 30, wakati Croatia itamenyana na Denmark Julai 1 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Newcastle vs Tottenham: Live score, team news and updates as Son Heung-min
waves goodbye after a decade in north London in a pre-season friendly
-
Follow Mail Sport's live blog for the latest score, team news and updates
as Newcastle take on Tottenham at the Seoul World Cup Stadium in a
pre-season fr...
17 minutes ago
0 comments:
Post a Comment